DESEMBA: Kwa maisha ya sala

Tuombe ili uhusiano wetu binafsi na Yesu Kristo uweze kutiwa nguvu na Neno la Mungu na maisha ya sala.

Pope Francis – Desemba 2020

Kitovu cha utume wa Kanisa ni sala.
Sala ni ufunguo kwetu sisi ili kuweza kuingia katika majadiliano na Baba.
Kila wakati tunaposoma sehemu fupi ya Injili tunamsikia Yesu akiongea nasi.
Tunakuwa na mazungumzo na Yesu.
Tunamsikiliza Yesu na tunamjibu.
Na hii ndio sala.
Kwa kusali, tunabadili hali halisi.
Na tunabadilisha mioyo yetu.
Mioyo yetu inabadilika tunaposali.
Tunaweza kufanya mambo mengi, lakini bila sala, hakuna kitakachofanya kazi.
Tuombe ili uhusiano wetu binafsi na Yesu Kristo uweze kutiwa nguvu na Neno la Mungu na maisha ya sala.
Katika ukimya, kila mmoja kwa moyo wa dhati wa sala.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – December 2020: For a life of prayer

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

La Machi Communication for Good Causes

Music production and mix by:

Índigo Music Design

Benefactors

adminDESEMBA: Kwa maisha ya sala