Kuhusu

Video ya Papa ni mpango rasmi wa kimataifa wa kusambaza nia za sala za kila mwezi za Baba Mtakatifu.  Mpango huu unafanywa na Mtandao wa Sala wa Baba Mtakatifu

Mtandao wa Sala wa Baba Mtakatifu ni kazi ya Kipapa.  Mtandao huu umepewa jukumu la kuhamasisha Wakatoliki kukabili changamoto za ulimwengu na za utume wa Kanisa, kwa njia ya sala na matendo mema.  Changamoto hizi hutolewa kila mwezi kwa Kanisa lote, kupitia nia za sala za Baba Mtakatifu

Utume wa Mtandao huu umejengeka katika mivuto na mialiko ya Moyo Mtakatifu wa Yesu: ni utume wa huruma kwa ulimwengu.  Ulianza mwaka 1984 kama “Utume wa Sala”.  Kwa sasa upo katika nchi zaidi ya 90 na unajumuisha zaidi ya Wakatoliki milioni 22. Utume huu unajumuisha tawi lake la vijana linaloitwa Vijana Wanaekaristia (EYM, Eucharistic Youth Movement).  Mwezi Desemba mwaka 2020, Baba Mtakatifu aliurasimisha utume huu kama Ushirika wa Kipapa wenye udhamini wa Vatikani, na akazindua katiba yake mpya, ambayo ilichapishwa katika ukamili wake mwezi Julai 2024. Mkurugenzi wake wa kimataifa ni Padre Cristóbal Fones, SJ.

Kwa habari zaidi, tembelea: popesprayer.va

Mradi unasaidiwa na Vyombo vya Habari vya Vatikani (Vatican Media)

 

Usage rights of “The Pope Video”
Attribution Non-Commercial No Derivatives (CC BY-NC-ND).
*Requires credits reference to the original author (The Pope Video – www.thepopevideo.org – by Pope’s Worldwide Prayer Network www.popesprayer.va).
**Does not allowed to be modify the work in any way.
***Does not allowed to use the work for commercial purposes.
For more information and other requests please contact: [email protected]

adminKuhusu