JANUARI | Kwa ajili ya haki ya kupata elimu

Tusali kuwaombea wahamiaji, wakimbizi na wale wanaoathirika na vita, kwamba haki yao ya kupata elimu, ambayo ni muhimu katika kujenga ulimwengu wenye utu zaidi, daima iheshimike.

NOVEMBA | Kwa wale waliopoteza mtoto

Tuwaombee wazazi wote wanaoomboleza kwa kufiwa na mtoto wa kiume au wa kike wapate usaidizi katika jamii yao, na wapate amani ya moyo kutoka kwa Roho wa Faraja.

OKTOBA | Kwa ajili ya umisionari wa wote

Tusali kuliombea Kanisa ili liendelee kudumisha mtindo-maisha wa kisinodi kwa kila namna, kama ishara ya uwajibikaji pamoja, na uendelezaji wa ushiriki, ushirika na umisionari mmoja kwa mapadre, watawa na walei.

SEPTEMBA | Kwa ajili ya kilio cha Dunia

Tusali ili kila mmoja wetu asikilize kwa moyo kilio cha Dunia yetu, na cha wahanga wa majanga ya kimazingira na mabadiliko ya hali ya hewa, tukijitoa binafsi kutunza ulimwengu tunamoishi.

TOTAL VIEWS

+ 240M

only in Vatican Networks

VIEWS 2024

+ 22M

PRESS ARTICLES

+ 28K

in 114 countries

Help spread the Pope’s Prayer Intentions today!

Nacho JimenezVideo ya Papa