SEPTEMBA: Kwa ajili ya uhusiano wetu na viumbe vingine vyote
Papa Leo XIV
Tusali ili, kwa kuhamasishwa na Mtakatifu Fransisko, tuwe na utambuzi wa mahusiano yetu na viumbe vyote vinavyopendwa na Mungu na vinavyostahili heshima na upendo.
Ee Bwana, unakipenda kila kitu ulichokiumba,
na hakuna chochote kilichopo nje ya fumbo la Upendo Wako.
Kila kiumbe, bila kujali udogo wake,
ni tunda la upendo Wako na kina nafasi yake hapa duniani.
Hata maisha madogo au mafupi, yanazungukwa na ulinzi Wako.
Kama Mtakatifu Fransisko wa Assisi, leo nasi tunataka kusema:
“Sifa kwako Wewe, Bwana wangu!”
Kwa kupitia uzuri wa uumbaji,
Unajifunua kwetu kama chanzo cha wema. Tunakuomba:
fungua macho yetu tuweze kukutambua,
tupate fundisho kupitia fumbo ya ukaribu Wako na viumbe vyote
kwamba dunia ni zaidi sana ya tatizo la kutatua.
Ni fumbo la kutafakari kwa shukrani na tumaini.
Tusaidie kugundua uwepo Wako katika viumbe vyote,
ili, tukilitambua hili kikamilifu,
tujisikie na kujua kwamba tuna wajibu wa kutimiza katika nyumba hii ya pamoja
ambapo unatualika kutunza, kuheshimu, na kulinda
maisha katika hali na mwonekano wake wote.
Sifa kwako Bwana!
Amina
Credits
Campaign title:
The Pope Video – SEPTEMBER | For our relationship with all of creation
A project by Pope’s Worldwide Prayer Network
In collaboration with Vatican Media
Creativity and co-production by:
Diego Angeli