Tuombe ili waamini wa dini mbalimbali waweze kushirikiana katika kutunza na kuendeleza amani, haki na udugu wa kibinadamu
Papa Leo XIV
Ewe Bwana Yesu,
Wewe uliye mmoja hata tunapokuona tofauti kwa macho yetu,
na unamtazama kila mtu kwa upendo,
tusaidie kutambuana kama ndugu, kaka na dada,
Tunaoitwa kuishi, kusali, kufanya kazi na kuwa na ndoto moja.
Tunaishi katika ulimwengu wenye uzuri mwingi,
lakini pia uliojeruhiwa kwa mafarakano makubwa.
Wakati mwingine dini, badala ya kutuunganisha,
zinakuwa chanzo cha mafarakano.
Tupe Roho Wako ili kutakasa mioyo yetu,
tuweze kutambua kile kinachotuunganisha
na, kutoka hapo, tujifunze tena jinsi ya kusikiliza
na kushirikiana bila kuleta uharibifu.
Tunaomba mifano halisi ya amani,
haki na udugu katika dini
Ituvutie kuamini kuwa inawezekana kuishi
na kufanya kazi pamoja, japokuwa tunatofautiana.
Dini zisitumike kama silaha au vitenganishi
bali ziwe madaraja na unabii:
zikiipa uhalisia ndoto ya kulinda manufaa ya wote,
kuendeleza maisha, kutunza tumaini
na kuwa chachu ya umoja katika ulimwengu uliogawanyika.
Amina.
Credits
Campaign title:
The Pope Video – OCTOBER | For collaboration between different religious traditions
A project by Pope’s Worldwide Prayer Network
In collaboration with Vatican Media
Creativity and co-production by:
La Machi