Tuwaombee wale wanaopambana na fikira za kujiua waweze kupata msaada, huduma na upendo wanaohitani katika jamii zao, na waone uzuri wa maisha.
Papa Leo XIV
Ee Bwana Yesu,
Wewe unayewaalika wanaolemewa na mizigo
waje Kwako na kupumzika ndani ya Moyo Wako,
mwezi huu tunawaombea kwako watu wote
wanaoishi katika giza la kukata tamaa,
hasa wale wanaopambana
na fikra za kujiua.
Tunawaombea daima wapate jumuiya
ambayo inawakaribisha, inawasikiliza na kuwapa usaidizi.
Nasi sote tupewe moyo msikivu na wenye huruma,
uwezao kutoa faraja na msaada,
na usaidizi wa kitaalamu unaohitajika.
Nasi tujue jinsi ya kuwa karibu nao kwa heshima na upole.
kusaidia kuponya majeraha, kuunganisha watu na kuondoa mipaka.
Pamoja tuweze kugundua kuwa maisha ni zawadi,
kwamba bado maisha yana uzuri na maana,
hata panapo maumivu na mateso.
Sote tunatambua vizuri kuwa wale wanaokufuasa Wewe
pia wanakabiliwa na huzuni na kukosa tumaini.
Tunakuomba daima utuonesha upendo Wako
ili kwamba, kupitia ukaribu wako nasi,
tunaweza kutambua na kutangaza kwa wote upendo wa Baba usio na mipaka,
anayetuongoza akitushika mkono tukiimarika katika imani yetu kwa maisha utupayo
Amina
Credits
Campaign title:
The Pope Video – NOVEMBER | For the prevention of suicide
A project by Pope’s Worldwide Prayer Network
In collaboration with Vatican Media
Creativity and co-production by:
The Roman Catholic Diocese of Phoenix