DESEMBA | Kwa ajili ya Wakristo walio kwenye maeneo yenye migogoro

Papa Leo XIV

Tuombe ili Wakristo wanaoishi kwenye maeneo yenye vita au migogoro, hasa Mashariki ya Kati, wawe mbegu za amani, mapatano na matumaini.

Ee Mungu wa amani,
ambaye kupitia damu ya Mwanao,
umeupatanisha ulimwengu na Nafsi Yako,
leo tunasali kuwaombea Wakristo
wanaoishi palipo na vita na vurugu.

Pale wanapozungukwa na maumivu,
tunaomba wasikose daima kuona wema wako kati wao,
na sala za kaka na dada zao katika imani.

Kwa kuwa ni katika Wewe tu, na wakiimarishwa na undugu,
ndipo wanaweza kuwa mbegu ya upatanisho,
wajenzi wa matumaini katika njia ndogo na kubwa kadhalika,
wanaweza kusamehe na kujongea mbele,
wakiwaleta pamoja waliotenganishwa,
na kutafuta haki bila kukosa huruma.

Ee Bwana Yesu, uliowaita wamebarikiwa
wale walio wapatanishi,
tufanye tuwe vyombo vyako vya amani
hata pale utulivu unapoonekana kuwa jambo lisilowezekana.

Ewe Roho Mtakatifu,
chanzo cha matumaini katika nyakati za giza tororo,
tunza imani ya wale wanaoteseka na imarisha matumaini yao.
Usiache tuwe watu wasiojali wengine,
ila tufanye wajenzi wa umoja, kama alivyofanya Yesu.

Amina

Credits

Campaign title:

The Pope Video – DECEMBER | For Christians in areas of conflict

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

DEVLMDESEMBA | Kwa ajili ya Wakristo walio kwenye maeneo yenye migogoro