Tuwaombee wazee, wawe walimu wa huruma ili uzoefu na hekima zao ziwasaidie vijana kutazama maisha yajayo kwa matumaini na wajibu.
Pope Francis – July 2022
Hatuwezi kuzungumza juu ya familia bila kuzungumza juu ya umuhimu wa wazee kati yetu.
Hatujawahi kuwa wengi miongoni mwetu katika historia ya ubinadamu, lakini hatujui vizuri namna ya kuishi hatua hii mpya ya maisha: kuna mipango mingi ya usaidizi, lakini uwepo wa miradi michache
Sisi wazee mara nyingi tuna hisia maalum kwa ajili ya huduma, kwa kutafakari, na kwa upendo. Sisi ni, au tunaweza kuwa walimu wa huruma. Kwa vipi!
Katika ulimwengu huu uliozoea vita, tunahitaji mapinduzi ya kweli ya huruma.
Katika hili, tuna wajibu mkubwa kwa vizazi vipya.
Tukumbuke: babu zetu na wazee ni mkate unaolisha maisha yetu, hekima iliyofichwa ya watu. Kwa hiyo, ni muhimu kuwasheherekea, na nimeanzisha siku maalumu kwa ajili yao.
Tuwaombee wazee, wawe walimu wa huruma ili uzoefu na hekima zao ziwasaidie vijana kutazama maisha yajayo kwa matumaini na wajibu.
Credits
Campaign title:
The Pope Video – July 2022: For the Elderly
A project by Pope’s Worldwide Prayer Network
In collaboration with Vatican Media
Creativity and co-production by:
La Machi Communication for Good Causes
Music production and mix by:
Benefactors
Benefactors:
Media partners:
Thanks to:
Dicastery for Laity, Family, and Life