OKTOBA | Kwa ajili ya umisionari wa wote

Tusali kuliombea Kanisa ili liendelee kudumisha mtindo-maisha wa kisinodi kwa kila namna, kama ishara ya uwajibikaji pamoja, na uendelezaji wa ushiriki, ushirika na umisionari mmoja kwa mapadre, watawa na walei.

Baba Mtakatifu – Oktoba 2024

Sisi Wakristo tuna wajibu juu ya utume wa Kanisa: Kila padre, kila mmoja.
Sisi mapadre si mabosi wa walei, bali wachungaji wao. Yesu alituita sisi na wengine—siyo sisi juu ya wengine, wala siyo sisi upande mmoja na wengine upande mwingine, bali wote pamoja katika hali ya kutoshelezana. Sisi ni jumuiya. Ndiyo maana inatupasa kutembea pamoja, tukichukua njia ya kisinodi.
Hakika unaweza kuniuliza, “Naweza kufanya nini mimi kama dereva wa basi? Mimi kama Mkulima, au Mvuvi?” Tunachopaswa kutenda wote ni kushuhudia kwa maisha yetu. Maisha yetu yaendane na utume wa Kanisa.
Walei wabatizwa wapo ndani ya Kanisa, ndani ya nyumba yao wenyewe na wanahitajika kuitunza. Hilo ni jukumu letu pia sisi makasisi na watu waliowekwa wakfu. Kila mtu anatoa mchango wake kupitia kila anachoweza kufanya vizuri zaidi. Tunawajibika pamoja katika umisionari mmoja, tunashiriki na kuishi katika ushirika mmoja wa Kanisa.
Tusali kuliombea Kanisa ili liendelee kudumisha mtindo-maisha wa kisinodi kwa kila namna, kama ishara ya uwajibikaji pamoja, na uendelezaji wa ushiriki, ushirika na umisionari mmoja kwa mapadre, watawa na walei.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – OCTOBER | For a shared mission

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

Benefactors

Thanks

Benefactors:

Pro Rete di preghiera del Papa

With the Society of Jesus

Synod, Prayer, Ministry, Jesus, Faith, Christ, Laity, Pastors, Priests, Journey of Faith, Community, Mission, Union, Church, Commitment, The Pope Video

Nacho JimenezOKTOBA | Kwa ajili ya umisionari wa wote