Tsali ili tuweze kujifunza jinsi ya kufanya maamuzi, kuchagua njia za uzima na kukataa kila kinachotutenganisha na Kristo na Injili.u
(Papa Leo XIV)
Roho Mtakatifu, Ewe nuru ya ufahamu wetu,
pumzi nyororo inayoongoza maamuzi yetu,
nijalie neema ya kuisikiliza sauti yako kwa umakini
na kuyatambua mapito yaliyofichika ya moyo wangu,
ili nipate kuyafahamu yaliyo hasa na maana kwako,
na kuuweka huru moyo wangu kutoka vifungo vya matatizo yake.
Ninakuomba neema ya kujifunza jinsi ya kutenga muda,
Ili kuchunguza jinsi ninavyotenda,
kutambua hisia zilizo ndani yangu,
na mawazo yanayonilemea
ambayo, mara nyingi nashindwa kuyatambua.
Ninatamani chaguzi zangu
ziniongoze kwenye furaha ya Injili.
Hata kama sharti nipitie wakati wa mashaka na uchovu,
hata kama ni lazima nipambane, nitafakari, nisake, na nianze upya…
Kwa sababu, mwisho wa safari,
faraja yako ni tunda la uamuzi sahihi.
Nijalie ufahamu wa kina wa kile kinachonisukuma kwa ndani,
ili nikatae kile kinachonitenga na Kristo.
na kumpenda na kumtumikia zaidi.
Amina.
Credits
Campaign title:
The Pope Video – JULY | For formation in discernment
A project by Pope’s Worldwide Prayer Network
In collaboration with Vatican Media
Creativity and co-production by:
DeSales Media
Ángela Cid
Ignacio Calfuquir