APRILI | Kwa matumizi ya teknolojia mpya

Tusali ili matumizi ya teknolojia mpya yasichukue nafasi ya uhusiano wa kibinadamu, yaheshimu utu wa binadamu na kutusaidia kukabili matatizo ya nyakati zetu.

Pope Francis – April 2025

Jinsi gani ningependa tupunguze kuangalia kwenye skrini na kuongeza kutazamana machoni!
Kuna jambo lisilo sawa kama tukitumia muda mwingi zaidi katika simu zetu za mkononi kuliko kuwa na watu. Skrini zinatufanya tusahau kuwa kuna watu nyuma yake wanaopumua, wanaocheka na kulia.
Ni kweli kwamba teknolojia ni matunda ya akili aliyotupa Mungu. Lakini tunapaswa kuitumia vema. Haipaswi kuwafaidisha wachache tu huku ikiwatenga wengine.
Tunapaswa kufanya nini basi? Tuitumie teknolojia kuunganisha na siyo kutenganisha watu. Tuitumie kuwasaidia maskini, kuboresha maisha ya wagonjwa na watu watu wenye uwezo tofauti. Tutumie teknolojia kuitunza dunia ambayo ni nyumba yetu ya pamoja. Teknolojia ituunganishe kama ndugu, kaka na dada.
Ni pale tunapotazamana machoni ndipo tunapogundua jambo pekee lenye maana: kuwa sisi ni kaka na dada, watoto wa Baba mmoja.
Tusali ili matumizi ya teknolojia mpya yasichukue nafasi ya uhusiano wa kibinadamu, yaheshimu utu wa binadamu na kutusaidia kukabili matatizo ya nyakati zetu.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – APRIL | For the use of the new technologies

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

adminAPRILI | Kwa matumizi ya teknolojia mpya