Tusali ili familia zenye mipasuko zipate tiba ya majeraha yao kupitia msamaha, na zione upya karama za kila mmoja, hata katika utofauti wa kila mtu.
Baba Mtakatifu – Machi 2025
Ni ndoto ya kila mtu kuwa katika familia nzuri na kamilifu. Hata hivyo hakuna kitu kama familia kamilifu. Kila familia ina matatizo yake, na furaha zake nyingi sana.
Kila mwanafamilia ni muhimu kwa sababu kila mtu ni tofauti na wengine, kila mtu ni wa kipekee. Lakini hizi tofauti zinaweza kusababisha migogoro na majeraha yenye maumivu.
Na dawa bora zaidi ya kuponya maumivu ya familia yenye majeraha ni msamaha.
Msamaha maana yake kupeana nafasi nyingine. Mungu anatufanyia hili kila wakati. Saburi ya Mungu haina mipaka. Mungu anatusamehe, anatunyanyua na kutupa mwanzo mpya. Msamaha daima unahuisha familia na kuifanya itazame mbele kwa matumaini.
Hata wakati ambapo hakuna uwezekano wa “mwisho wenye furaha” ambao tunaupendelea, neema ya Mungu inatupa nguvu ya kusamehe, pia huleta amani kwa sababu inatuweka huru kutokana na huzuni, na kututoa kwenye kifungo cha chuki.
Tusali ili familia zenye mipasuko zipate tiba ya majeraha yao kupitia msamaha, na zione upya karama za kila mmoja, hata katika utofauti wa kila mtu.
Credits
Campaign title:
The Pope Video – MARCH | For families in crisis
A project by Pope’s Worldwide Prayer Network
In collaboration with Vatican Media
Creativity and co-production by:
Gaia Valeria Rosa and Diego Angeli