FEBRUARI | Kwa ajili ya miito ya upadre na utawa

Tusali kuliombea Kanisa ili liweze kupokea tamaa na mashaka ya vijana wale wanaojisikia kuitwa kuishi utume wa Yesu maishani, kwa njia ya maisha ya kikuhani au maisha ya kitawa.

Baba Mtakatifu – Februari 2025

Nilipowa na umri wa miaka 17, nilikuwa nasoma na nafanya kazi. Nilikuwa na mipango yangu mwenyewe. Sikuwa nawazia hata kidogo kuwa padre. Lakini siku moja, niliingia kanisani…na Mungu alikuwa hapo, akiningoja!
Mungu bado anawaita vijana hata leo, wakati mwingine kwa njia ambazo hata hatuwezi kufikiria. Wakati mwingine hatumsikii Mungu kwa sababu tunajishughulisha sana na mambo yetu wenyewe, mipango yetu wenyewe, hata pia na mambo yetu wenyewe katika Kanisa.
Lakini Roho Mtakatifu pia anasema nasi kwa njia ya ndoto, na anazungumza nasi kupitia mahangaiko wanayopitia vijana mioyoni mwao. Tukitembea pamoja nao katika safari zao, tutaona jinsi Mungu anavyowashirikisha kufanya mambo mapya. Hapo tutaweza kupokea wito wake kwa njia ambazo unaweza hutumikia vyema Kanisa na ulimwengu wa leo.
Tuwaamini vijana! Na, zaidi ya yote, tumwamini Mungu kwa kuwa ndiye anayemwita kila mtu!
Tusali kuliombea Kanisa ili liweze kupokea tamaa na mashaka ya vijana wale wanaojisikia kuitwa kuishi utume wa Yesu maishani, kwa njia ya maisha ya kikuhani au maisha ya kitawa.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – FEBRUARY | For vocations to the priesthood and religious life

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

Benefactors

Thanks to

+ José H. Gómez, Archbishop of Los Angeles 

Sarah Yaklic

Isabel Cacho

Peter Lobato

John Rueda 

Office for Religious Education – Archdiocese of Los Angeles

Office for Vocations – Archdiocese of Los Angeles

Francesca Ambrogetti

With the Society of Jesus

adminFEBRUARI | Kwa ajili ya miito ya upadre na utawa