Tusali kuwaombea wahamiaji, wakimbizi na wale wanaoathirika na vita, kwamba haki yao ya kupata elimu, ambayo ni muhimu katika kujenga ulimwengu wenye utu zaidi, daima iheshimike.
Baba Mtakatifu – Januari 2025
Leo tunapitia “janga la kielimu.” Kusema hivi siyo kutia chumvi hata kidogo. Kwa sababu ya vita, uhamiaji na umaskini, wavulana na wasichana wapatao milioni 250 wanakosa elimu.
Watoto na vijana wote wana haki ya kwenda shule, bila kujali hali yao ya uhamiaji.
Elimu ni tumaini kwa kila mmoja – inaweza kuokoa wahamiaji na wakimbizi kutokana na ubaguzi, mitandao ya kihalifu, na unyonyaji…. Watoto wengi sana wananyonywa! Elimu inaweza kuwasaidia kufanywa sehemu ya jumuiya zinazowapokea.
Elimu hufungua milango ya maisha bora zaidi ya baadaye. Kwa namna hii, wahamiaji na wakimbizi wanaweza kutoa mchango wao kwa jamii, katika nchi yao mpya au katika nchi yao ya asili, ikiwa wataamua kurudi.
Tena tusisahau kamwe kwamba yeyote anayemkaribisha mgeni, anamkaribisha Yesu Kristo.
Tusali kuwaombea wahamiaji, wakimbizi na wale wanaoathirika na vita, kwamba haki yao ya kupata elimu, ambayo ni muhimu katika kujenga ulimwengu wenye utu zaidi, daima iheshimike.
Credits
Campaign title:
The Pope Video – JANUARY | For the right to an education
A project by Pope’s Worldwide Prayer Network
In collaboration with Vatican Media
Creativity and co-production by:
Gaia Valeria Rosa, Diego Angeli, and Andrea Schneider Graziosi
Benefactors
Thanks to
Raúl De La Fuente
Fondazione AVSI – People for development
Associazione Comunità Papa Giovanni XXIII
Istituto Madre Asunta Tijuana Mexico
Marco Palombi
© UNICEF – HIS: Ukrainian teaching assistants play a vital role in Czech schools – Yana’s story
© UNICEF – UNICEF Spokesperson James Elder visits Ukraine – 2024
© UNICEF NYHQ Teacher Anastasiia – Ukrainian children in Romania
UNICEF/Chiari/Trovato/2024
UNICEF/Anicito/2024
Benefactors
With the Society of Jesus
Right to Education, Migrants, Refugees, Hope Through Education