DESEMBA | Kwa ajili ya mahujaji wa matumaini

Tusali ili Jubilei iliyo mbele yetu ituimarishe katika imani yetu, ikitusaidia kumtambua Kristo Mfufuka katika ya maisha yetu, akitufanya kuwa mahujaji wa tumaini la Kikristo.

Baba Mtakatifu – Desemba 2024

Tumaini la Kikristo ni zawadi ya Mungu inayoyajazia furaha maisha yetu.
Na leo tumaini hilo tunalihitaji sana. Hakika ulimwengu unalihitaji sana.
Wakati ambapo hujui iwapo kesho utaweza kulisha watoto wako, au ikiwa unachosomea kitakuwezesha kupata kazi nzuri, ni rahisi kukata tamaa.
Ni wapi tunapoweza kutafuta tumaini?
Tumaini ni kama nanga – nanga ambayo tunaishusha kwa kamba ili tubaki ufukweni.
Inabidi tushikilie kamba ya tumaini bila kulegeza mikono.
Tusaidiane kukutana na Kristo anayetupa maisha, na tuianze safari kama mahujaji wa tumaini katika kuyafurahia hayo maisha. Kuingia katika Jubilei ijayo ni hatua moja mbele katika hayo maisha.
Siku kwa siku, tuyajaze maisha yetu kwa zawadi ya tumaini atupalo Mungu, na kupitia kwetu, turuhusu tumaini hilo liwafikie wote wanaolitafuta.
Tusisahau kuwa tumaini halikatishi tamaa.
Tusali ili Jubilei iliyo mbele yetu ituimarishe katika imani yetu, ikitusaidia kumtambua Kristo Mfufuka katika ya maisha yetu, akitufanya kuwa mahujaji wa tumaini la Kikristo.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – DECEMBER | For pilgrims of hope

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

Pilgrims, Jubilee2025, Church, Hope, Community, The Pope Video, Prayer Intention, Click To Pray

adminDESEMBA | Kwa ajili ya mahujaji wa matumaini