NOVEMBA | Kwa wale waliopoteza mtoto

Tuwaombee wazazi wote wanaoomboleza kwa kufiwa na mtoto wa kiume au wa kike wapate usaidizi katika jamii yao, na wapate amani ya moyo kutoka kwa Roho wa Faraja.

Baba Mtakatifu – Novemba 2024

Tunaweza kusema nini kwa wazazi waliofiwa na mtoto? Tunaweza kuwafariji vipi?
Hakuna maneno yoyote.
Mwanandoa anapofiwa na mwenzi wake, anakuwa mgane au mjane. Mtoto anayefiwa na mzazi anakuwa yatima. Kuna neno la kuwataja. Lakini mzazi anapofiwa na mtoto, hakuna neno la kumtaja. Maumivu ni makubwa sana, hata hakuna neno la kuelezea.
Tena si kawaida mtoto kufariki kabla ya mzazi wake. Maumivu yanayosababishwa na pengo hili ni makali kupita kiasi.
Maneno ya kutia moyo wakati mwingine hayana uhalisia, hayasaidii lolote. Japokuwa yanazungumzwa kwa nia nzuri kabisa, yanaweza kukuza kidonda.
Kuwaliwaza hawa wazazi waliopoteza mtoto, inatupasa kuwasikiliza, kuwa karibu nao kwa upendo, kujali uchungu wanaopitia, tukimwiga Yesu Kristo jinsi alivyowafariji waliokuwa na huzuni.
Tena, wale wazazi walio imara katika imani yao, bila shaka wanaweza kupata faraja kutoka katika familia nyingine ambazo baada ya kuteseka kwa msiba mbaya kama huu, wamejikuta wamezaliwa upya katika matumaini.
Tuwaombee wazazi wote wanaoomboleza kwa kufiwa na mtoto wa kiume au wa kike wapate usaidizi katika jamii yao, na wapate amani ya moyo kutoka kwa Roho wa Faraja.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – NOVEMBER | For those who have lost a child

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

Benefactors

Thanks to

Don Luigi Verdi
Luca Valdiserri
Paola Di Caro
Ama – Cimitero Monumentale del Verano

With the Society of Jesus

Children, Family, Parents, Loss, Grief, The Pope Video, Prayer Intention, Click To Pray, We Pray Together, Holy Spirit

adminNOVEMBA | Kwa wale waliopoteza mtoto