MEI | Kwa ajili ya malezi ya watawa wa kike na wa kiume, na waseminari

Tuwaombee watawa wa kike na wa kiume, na waseminari, ili wakue katika safari ya miito yao kupitia malezi ya kiutu, kichungaji, kiroho na kijumuiya wanayopata kuwafanya kuwa mashahidi wa kuaminika wa Injili.

Baba Mtakatifu – MEI 2024

Kila utume ni kama almasi toka mgodini, inayohitaji kusafishwa, kufanyiwa kazi na kukatwa katika umbo linalohitajika.
Kasisi au sista mzuri, zaidi ya yote sharti awe mtu aliyelelewa, kufundwa na kufanywa na neema ya Mungu; ni watu wanaotambua mapungufu yao binafsi, na wapo tayari kuishi maisha ya sala na ya kujitolea kabisa kuishuhudia Injili.
Kuanzia seminari na novisiati, matayarisho yao sharti yafanywe kikamilifu, na yahusiane moja kwa moja na maisha ya watu wengine.
Malezi ya watawa na makasisi hayaishi katika muda fulani, ila huendelea maisha yote, yakimjengea mtu umoja wa nafsi kiakili, kiutu, kihisia, kiroho.
Pia kuna matayarisho ya kuishi katika jumuiya – maisha ya jumuiya yana manufaa sana, japokuwa yanaweza kuwa magumu wakati mwingine.
Kuishi pamoja si sawa na kuishi katika jumuiya.
Tuwaombee watawa wa kike na wa kiume, na waseminari, ili wakue katika safari ya miito yao kupitia malezi ya kiutu, kichungaji, kiroho na kijumuiya wanayopata kuwafanya kuwa mashahidi wa kuaminika wa Injili.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – MAY | For the formation of men and women religious, and seminarians

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

Benefactors

Vocation, Vocations, Seminarians, Men Religious, Women Religious, Nuns, Sisters, Formation, The Pope Video, Prayer Intention, Click To Pray

fiorellaMEI | Kwa ajili ya malezi ya watawa wa kike na wa kiume, na waseminari