DESEMBA | Makatekista

Tuwaombee makatekista, walioitwa kutangaza Neno la Mungu: wawe mashahidi wa neno hilo, kwa ujasiri na kwa kipaji cha kubuni na kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, kwa furaha na amani kubwa.

Pope Francis – December 2021

Makatekista wana umuhimu mkubwa sana katika kusambaza na kukua kwa imani.
Utume wa mlei wa katekista ni wito; ni utume. Kuwa katekista ina maana kuwa wewe “ni katekista”, na si kwamba “unafanya kazi kama katekista”. Ni namna yote ya kuwa, na tunahitaji makatekista wazuri ambao ni marafiki na walimu.
Tunahitaji watu wenye kipaji cha ubunifu ambao watatangaza Injili si kwa ukimya wala kwa sauti kubwa, bali kwa maisha yao, kwa upole, kwa lugha mpya na kwa kufungua njia mpya.
Katika majimbo mengi, kwenye mabara mengi, kimsingi, uinjilishaji upo mikononi mwa katekista.
Tuwashukuru makatekista kwa shauku lao la ndani ambalo linawawezesha kuuishi utume huu kwa ajili ya huduma ya Kanisa.
Tuwaombee makatekista, walioitwa kutangaza Neno la Mungu: wawe mashahidi wa neno hilo, kwa ujasiri na kwa kipaji cha kubuni na kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, kwa furaha na amani kubwa.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – December 2021: Catechists

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

Gaia Valeria Rosa, Diego Angeli and Andrea Schneider Graziosi

Music production and mix by:

Índigo Music Design

Benefactors

Media partners:

Aleteia

Thanks to:

Paolo “Gojo” Colasanti
Parrocchia Nostra Signora di Coromoto – Roma

With the Society of Jesus

Katekista makatekista, ubunifu, wito, utume, kusambaza imani, ushuhuda, lugha mpya, uinjilishaji.

adminDESEMBA | Makatekista