Tuwaombee wale walio pembezoni mwa jamii katika maisha ya chini ya kibinadamu, Hali zao, ili wasitelekezwe na taasisi mbalimbali na kamwe wasitupwe nje.
Pope Francis – September 2023
Mtu asiye na makazi anayekufa barabarani hatatokea kamwe miongoni mwa hadithi za juu kwenye mitambo ya udukuzi au matangazo ya habari.
Je, tungewezaje kufikia kiwango hiki cha kutojali?
Inakuwaje kwamba tunaruhusu “utamaduni wa kutupa” – kwayo mamilioni ya wanaume na wanawake hawana thamani yeyote ikilinganishwa na bidhaa za kiuchumi – ni jinsi gani tunaruhusu utamaduni huu wa kutawala maisha yetu, miji yetu, mfumo wetu wa maisha?
Shingo zetu zitakuwa ngumu kutokana na kuangalia upande mwingine ili tusiwe na ulazima wa kutazama uhalisia huu.
Tafadhali, tuache kuwafanya waliomo pembezoni mwa jamii wasionekane, hata kama ni kutokana na umaskini, uraibu, ugonjwa wa akili au ulemavu.
Hebu tuzingatie kuwakubali, kuwakaribisha watu wote wanaohitaji.
“Utamaduni wa kukaribisha,” ukarimu, kutoa makazi, kutoa nyumba, kutoa upendo, kutoa joto la kibinadamu.
Tuwaombee wale walio pembezoni mwa jamii katika maisha ya chini ya kibinadamu, Hali zao, ili wasitelekezwe na taasisi mbalimbali na kamwe wasitupwe nje.
Credits
Campaign title:
The Pope Video – September 2023: For people living on the margins