AGOSTI | Kwa Siku ya Vijana Ulimwenguni

Tuombe kwamba Siku ya Vijana Ulimwenguni huko Lisbon iwasaidie vijana waanze safari, wakishuhudia Injili kwa maisha yao wenyewe.

Baba Mtakatifu – Agosti 2023

Ninapoenda Kanisani katika mtaani kwangu, naona wazee tu. Je, Kanisa ni la wazee pekee?

Kanisa si klabu ya wazee zaidi ya klabu ya vijana. Likiwa ni kwa ajili ya wazee, itakufa. Mtakatifu Yohane Paulo wa II aliwahi kusema kuwa ukiishi na vijana unakuwa kijana mwenyewe. Kanisa linahitaji vijana ili lisizeeke.

Mpendwa Papa Francisko, kwa nini ulichagua mada, “Mariamu akaondoka na kwenda kwa haraka” kwa hii SVU?

Kwa sababu mara tu Mariamu alipojua kwamba atakuwa mama wa Mungu, hakukaa hapo akipiga “selfie” au kujionyesha. Jambo la kwanza alilofanya ni kuingia barabarani, kwa haraka, kuhudumu, kusaidia. Wewe pia inabidi ujifunze kutoka kwake ili uwe njiani kuwasaidia wengine.

Ni nini matumaini yako kwa SVU huko Lisbon?

Huko Lisbon, ningependa kuona mbegu kwa siku zijazo za ulimwengu. Ulimwengu ambao upendo uko katikati, ambapo tunaweza kuhisi kuwa sisi ni ndugu. Tupo vitani; tunahitaji kitu kingine. Ulimwengu ambao hauogopi kushuhudia Injili. Ulimwengu wenye furaha – kwa sababu ikiwa sisi Wakristo hatuna furaha, hatuaminiki, hakuna mtu atakayetuamini.

Tuombe kuwa Siku ya Vijana Ulimwenguni huko Lisbon, itusaidie sisi vijana kuanza safari, tukishuhudia Injili kwa maisha yetu wenyewe.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – August 2023: For World Youth Day

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

La Machi Communication for Good Causes

Benefactors

Thanks to:

National offices of the Pope’s Worldwide Prayer Network and its youth branch EYM in Guatemala, Filipinas and Ivory Coast.

With the Society of Jesus

adminAGOSTI | Kwa Siku ya Vijana Ulimwenguni