MEI | Kwa mazingira ya kazi

Tuombe ili kwamba, kupitia kazi, kila mtu apate utoshelevu, familia zidumu katika heshima kiutu, na jamii ziwe za kibinadamu zaidi.

Mei 2025

Katika uchapishaji wake wa kila mwaka wa nia za sala kwa 2025, Papa Fransisko alitualika mwezi Mei tusali kwa ajili ya mazingira ya kazi.

Mtandao wa Sala wa Baba Mtakatifu Ulimwenguni unautolea kwa Mungu utume wa Papa Mpya na unaendelea na kazi yake ya kitume ya kuweka mbele ya Mungu changamoto za wanadamu na za utume wa Kanisa.

Mwezi huu tuhamasishwe kusali na video hii yenye maneno ya mapapa watatu waliopita: Fransisko, Benedikto XVI, na Mtakatifu Yohane Paulo II.

Katika wa Hadhira Kuu mwaka 2022, Papa Fransisko alisema: Wainjili Matayo na Marko wanamtaja Yosefu kama “seremala”.  Yesu alifanya kazi ya baba yake iliyokuwa ngumu sana. Kwa mtazamo wa kiuchumi, haikuhakikishia kipato kikubwa Ukweli huu wa wasifu wa Yosefu na Yesu unanifanya nifikirie juu ya wafanyakazi wote ulimwenguni.”

Kazi,” anaongeza Papa Fransisko, “ni chemchemi ya heshima ya mtu. Kinachokupa heshima siyo kuleta chakula nyumbani.”

Papa Benedikto XVI, akihutubia wafanyakazi wote kwenye sikukuu ya Mtakatifu Yosefu mwaka 2006, pia alisisitiza kwamba “kazi ni muhimu sana kwa ukamilifu wa mwanadamu na maendeleo ya jamii. Kwa hivyo, sharti wakati wote kazi ipangwe na kutekelezwa kwa heshima kamili kwa utu wa binadamu, tena lazima iwe kwa faida ya wote.”  Wakati huo huo, Papa Benedikto alisema, “ni muhimu kwamba watu wasikubali kuwa watumwa wa kazi au waabudu-kazi, wakidai kupata ndani yake maana ya juu na dhahiri kabisa ya maisha.”

Na Mtakatifu Yohane Paulo II wakati wa Jubilei ya Wafanyakazi katika mwaka wa 2000 alisema kwamba, “Mwaka wa Jubilei unahitaji ugunduzi mpya wa maana na thamani ya kazi. Pia ni mwaliko wa kushughulikia usawa wa kiuchumi na kijamii katika ulimwengu wa kazi kwa kupanga upya mpangilio wa thamani, kuweka kipaumbele kwa utu wa wanaume na wanawake wanaofanya kazi na kwa uhuru wao, uwajibikaji na ushiriki wao.” Mt. Yohane Paulo II pia alituhimiza “kuondoa dhuluma,” bila kuwasahau wale “wanaoteseka kwa sababu ya ukosefu wa ajira, mishahara duni au ukosefu wa rasilimali.”

Tuombe ili kwamba, kupitia kazi, kila mtu apate utoshelevu, familia zidumu katika heshima kiutu, na jamii ziwe za kibinadamu zaidi.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – MAY | For working conditions

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

adminMEI | Kwa mazingira ya kazi