AGOSTI | Kwa ajili ya kuendeleza maisha ya pamoja

Tusali kuziombea jamii ambazo zinakabiliwa zaidi na ugumu wa kuishi pamoja, kwamba zisiangushwe na kutokomezwa na vishawishi vya ukabila, udini au tofauti za kisiasa na kiitikadi.

Papa Leo XIV

Ee Yesu, Bwana wa historia yetu,
Rafiki mwaminifu na uwepo hai,
Wewe usiyechoka kuja kukutana nasi,
Tunakuja mbele yako, kuomba Yako amani,

Tunaishi katika nyakati za hofu na mgawanyiko.
Wakati mwingine tunatenda kana kwamba tuko peke yetu,
Tunajenga kuta kututenga sisi kwa sisi,
Tukisahau kuwa sisi ni ndugu, ni kaka na dada.

Tushushie Roho Wako, Ee Bwana,
Kuwasha ndani yetu
Hamu ya kusikilizana na kuelewana,
Kuishi pamoja kwa heshima na huruma.

Tupe uthubutu wa kutafuta njia za mazungumzo,
Kuwa na miitikio ya kidugu kukabiliana na mizozo,
Kufungua mioyo yetu kwa wengine bila woga wa mitazamo tofauti.

Tufanye wajenzi wa madaraja,
Tuweze kushinda mipaka na vizingiti vya kiitikadi,
Tuweze kuwaona wengine kupitia macho ya moyoni,
Na kutambua ndani ya kila mtu heshima isiyofutika.

Tusaidie kutengeneza nafasi ambapo tumani linaweza kustawi,
Mahali ambapo kuwa tofauti si tishio kwa yeyote,
Bali utajiri wa kutufanya wanadamu zaidi.

Amina.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – AUGUST | For mutual coexistence

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

Benefactors

adminAGOSTI | Kwa ajili ya kuendeleza maisha ya pamoja