DESEMBA | Kwa watu wenye ulemavu

Tuombe kwamba watu wenye ulemavu wawe katikati ya uangalizi katika jamii, ili taasisi ziweze kutoa mpango jumuishi unaothamini ushiriki wao kamilifu.

Baba Mtakatifu – Desemba 2023

Watu wenye ulemavu ni miongoni mwa watu dhaifu sana miongoni mwetu.
Baadhi yao hukataliwa, kutokana na ujinga, unaotokana na ubaguzi, ambao unawatenga.
Taasisi za kiraia zinahitaji kusaidia miradi yao kupitia upatikanaji wa elimu, ajira, na mahali ambapo wanaweza kuonyesha ubunifu wao.
Mipango na mikakati inahitajika ili kukuza ushirikishwaji wao.
Zaidi ya yote, mioyo mikubwa inahitajika kwa wanaotaka kuandamana nao.
Inamaanisha kubadili mtizamo wa fikra zetu kidogo na kujifungua wenyewe kwa uwezo na vipaji vya hawa watu wenye uwezo tofauti, katika jamii na pia katika maisha ya Kanisa.
Na hivyo, kuunda parokia inayofikiwa kabisa haimaanishi tu kuondoa vikwazo vya kimwili. Pia inamaanisha kwamba tuache kuwachukulia kama “wao” na kuanza kuzungumza juu ya “sisi”.
Tuombe kwamba watu wenye ulemavu wawe katikati ya uangalizi katika jamii, ili taasisi ziweze kutoa mpango jumuishi unaothamini ushiriki wao kamilifu.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – December 2023: For people with disabilities

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

Benefactors

Benefactor:

Thanks to:

Comunità di Sant’Egidio
Comitato Italiano Paralimpico
Dicastero per i Laici, la Famiglia e la Vita
Trattoria degli Amici
Museo Laboratorio d’Arte Tor Bella Monaca Roma
POTIPICTURES

With the Society of Jesus

Inclusion, Persons with disabilities, Disability, The Pope Video, Pope Francis, Prayer Intention, Click To Pray

fiorellaDESEMBA | Kwa watu wenye ulemavu