Juni | Uzuri wa Ndoa

Na tuwaombee vijana wanaojiandaa kwa ndoa kwa fadhila za Jumuiya za Kikristo: wakue katika upendo, ukarimu, na uvumilivu.

Pope Francis – June 2021

Je, ni kweli wasemavyo baadhi ya watu—kuwa vijana hawataki kufunga ndoa hasa katika muda huu wenye magumu?
Kufunga ndoa na kushiriki maisha pamoja ni jambo zuri na la kupendeza
Ni safari yenye kuhitaji umakini mkubwa, wakati mwingine ngumu, na wakati mwingine inatatiza, lakini ina matokeo mazuri kustahilisha kuifanyia bidii. Na kwenye safari hii ndefu ya maisha, mume na mke hawapo peke yao. Yesu huambatana nao.
Ndoa si tendo la “kijamii” tu; ni wito wenye chimbuko lake moyoni; ni uamuzi makini kwa ajili ya maisha yote, hivyo unahitaji maandalizi maalumu.
Tafadhali, kamwe usisahau hili: Mungu ana ndoto kwa ajili yetu—upendo—na anatusihi tuipokee na kuifanya ndoto hii kuwa yetu.
Tuupokee uwe wetu huo upendo ambao ni ndoto ya Mungu kwa ajili yetu.
Na tuwaombee vijana wanaojiandaa kwa ndoa kwa fadhila za Jumuiya za Kikristo: wakue katika upendo, ukarimu, na uvumilivu. Hii ni kwa kuwa uvumilivu wa hali ya juu ni hitaji lisilokwepeka ili kupenda. Lakini matokeo yake si mema?

Credits

Campaign title:

The Pope Video – June 2021: The beauty of marriage

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

Gaia Valeria Rosa, Diego Angeli and Andrea Schneider Graziosi

Music production and mix by:

Índigo Music Design

Harusi, wito kwenye ndoa, uzuri wa ndoa, Bwana, Bibi harusi, mwenzi, mume

adminJuni | Uzuri wa Ndoa