JULAI | Urafiki wa Kijamii

Tuombe, ili kwenye jamii, uchumi na katika hali ya siasa ya mtafaruku tuweze kuwa na ujasiri na shauku ya ujenzi wa majadiliano na urafiki.

Pope Francis – July 2021

Biblia inasema ampataye rafiki amepata hazina.
Napenda kumwalika kila mmoja kuvuka mpaka na kwenda nje ya makundi ya marafiki na kujenga urafiki wa kijamii, ambao ni muhimu sana katika kuishi pamoja.
Tunahitaji zaidi kuwa na makabiliano mapya na masikini na wenye kuweza kudhuriwa, na wale walio pembezoni. Na pia tunahitaji kujiweka mbali na mifumo ya serikali/siasa inayowatumia watu katika machungu yao bila kutoa suluhisho, huku ikipendekeza fumbo ambalo halisuluhishi chochote.
Ni lazima tuukimbie kabisa uadui wa kijamii ambao huharibu na kuacha mgawanyiko.
Na hili si rahisi sikuzote, hasa nyakati zetu ambapo sehemu ya siasa, jamii na vyombo vya habari vina mwelekeo wa kujenga maadui ili kuwashinda katika mashindano ya madaraka.
Majadiliano ni njia ya kuona uhalisia katika namna nyingine, ili tuweze kuishi kwa shauku changamoto tunazokabiliana nazo katika kujenga maslahi ya umma.
Tuombe, ili kwenye jamii, uchumi na katika hali ya siasa ya mtafaruku tuweze kuwa na ujasiri na shauku ya ujenzi wa majadiliano na urafiki, wanaume na wanawake ambao daima tunadumu katika kusaidia na hatuachi nafasi ya uadui au vita.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – July 2021: Social friendship

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

La Machi

Music production and mix by:

Índigo Music Design

adminJULAI | Urafiki wa Kijamii