Mei: Ulimwengu wa fedha

Na tuombe ili wale walio na dhima ya fedha washirikiane na serikali kudhibiti eneo la fedha na kuwalinda wananchi dhidi ya hatari zake.

Pope Francis – May 2021

Uchumi wa kweli, ambao unatengeneza ajira, upo katika kipeo cha mgogoro. Ni watu wangapi ambao hawana ajira!- Lakini masoko ya fedha hayajawahi kuongezeka kama yalivyo sasa hivi.
Ulimwengu wa juu wa fedha upo umbali gani kutoka kwenye maisha ya watu wa kawaida!
Kama fedha haitadhibitiwa, itakuwa ni dhahania zinazoendeshwa na sera mbalimbali za kifedha.
Hali hii si endelevu. Na ni hatari.
Ili masikini wasisumbuke na madhara ya maumivu ya mfumo huu, dhahania ya kifedha ni lazima idhibitiwe kwa uangalifu.
Dhahania. Nataka kulitia mkazo neno hilo.
Fedha iwe aina ya mfumo wa huduma na chombo cha kuwahudumia watu na kuwatunza katika makao ya pamoja.
Bado tuna muda wa kuanza mchakato huu wa mbadiliko ya dunia! Kuifanyia kazi aina nyingine ya uchumi, ambao ni wa haki, wa pamoja na wa kudumu.
Tunaweza kulifanya hili! Na tuombe ili wale walio na dhima ya fedha washirikiane na serikali kudhibiti eneo la fedha na kuwalinda wananchi dhidi ya hatari zake.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – May 2021: The world of finance

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

La Machi

Music production and mix by:

Índigo Music Design

Uchumi wa kifedha, ulimwengu wa fedha, dhahania, masoko ya fedha, udhibiti wa masoko ya fedha, nguvu za kiuchumi.

adminMei: Ulimwengu wa fedha