Aprili: Haki za Msingi

Tuwaombee wale wanaohatarisha maisha yao kwa kupigania haki za msingi chini ya udikteta, utawala wa kimabavu na hata kwenye matatizo ya kidemokrasia, ili waweze kuona kujitolea kwao nan a kazi yao inazaa matunda mengi.

Pope Francis – April 2021

Kutetea haki za msingi za binadamu kunahitaji ujasiri na ushupavu.
Ninazungumzia kupambana kikamilifu na umasikini, ukosefu wa usawa, ukosefu wa kazi, nyumba na malazi na kunyimwa kwa haki za jamii na za kazi.
Mara nyingi, haki za msingi za binadamu hazipo sawa kwa wote.
Kuna wa daraja la kwanza, la pili na la tatu, na wale ambao ni wa kutupika
Hapana. Ni lazima ziwe sawa kwa wote.
Katika baadhi ya sehemu, kutetea utu wa watu kunaweza kumaanisha kwenda jela, bila kuhukumiwa.
Kila binadamu ana haki ya kukua kikamilifu, na haki zake za msingi haziwezi kunyimwa na nchi yoyote.
Tuwaombee wale wanaohatarisha maisha yao kwa kupigania haki za msingi chini ya udikteta, utawala wa kimabavu na hata kwenye matatizo ya kidemokrasia, ili waweze kuona kujitolea kwao nan a kazi yao inazaa matunda mengi.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – April 2021: Fundamental Rights

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

La Machi

Music production and mix by:

Índigo Music Design

adminAprili: Haki za Msingi