MACHI | Kwa ajili ya mashahidi wa siku zetu, mashahidi wa Kristo

Tuombe kwamba wale wanaohatarisha maisha yao kwa ajili ya Injili katika sehemu mbalimbali za dunia waweze kulijaza Kanisa kwa ujasiri na msukumo wao wa kimisionari.

Baba Mtakatifu – MACHI 2024

Mwezi huu, ninataka kukuambia hadithi ambayo ni onyesho la Kanisa la leo. Ni hadithi ya ushuhuda mdogo wa imani.
Nilipotembelea kambi ya wakimbizi huko Lesbos, mwanamume mmoja aliniambia, “Baba, mimi ni Mwislamu. Mke wangu alikuwa Mkristo. Magaidi walikuja kwetu, wakatutazama na kutuuliza ni dini gani. Walimsogelea mke wangu wakiwa na msalaba na kumwambia autupe chini. Hakufanya hivyo, na wakamkata koo mbele yangu.” Ndicho kilichotokea.
Najua hakuwa na kinyongo. Upendo wa mke wake ulikuwa kielelezo kwake,  ni upendo kwa Kristo ambao ulimfanya akubali, na kuwa mwaminifu hadi kufa.
Ndugu zangu, daima kutakuwa na wafia imani miongoni mwetu. Hii ni ishara kwamba tuko kwenye njia sahihi.
Mtu anayejua aliniambia kuna wafia imani wengi leo kuliko mwanzo wa Ukristo.
Ujasiri wa mashahidi, ushuhuda wa mashahidi, ni baraka kwa kila mtu.
Tuombe kwamba wale wanaohatarisha maisha yao kwa ajili ya Injili katika sehemu mbalimbali za dunia waweze kulijaza Kanisa kwa ujasiri na msukumo wao wa kimisionari. Na kuwa wazi kwa neema ya kifo cha kishahidi.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – MARCH For the martyrs of our day, witnesses to Christ

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media and ACN International

Creativity and co-production by:

Martyrs, Witness of Faith, Persecuted Christians, Church, The Pope Video, Prayer Intention, Click To Pray, We Pray Together, Holy Spirit

fiorellaMACHI | Kwa ajili ya mashahidi wa siku zetu, mashahidi wa Kristo