JANUARI | Ubaguzi na ukandamizaji wa kidini

Tusali ili wale wanaobaguliwa na kukandamizwa kwa sababu za kidini waweze kupata ndani ya jamii wanamoishi haki na heshima ya kiutu inayotokana na kuwa kaka na dada.

Pope Francis – January 2022

Inawezekanaje kuwa waumini wa dini zenye idadi ndogo ya watu kwa sasa wanabaguliwa na kukandamizwa.
Tunawezaje kuruhusu katika jamii hii, ambayo imestaarabika hivi, pakawepo watu wanaokandamizwa kwa sababu pekee ya kwamba wanaiungama imani yao hadharani? Siyo tu kwamba jambo hili halikubaliki; ni kinyume cha ubinadamu, ni wendawazimu.
Uhuru wa imani hauishii kwenye uhuru wa kuabudu peke yake—yaani, kwamba watu wanaweza kukusanyika kwa ajili ya kuabudu katika siku iliyoainishwa na vitabu vyao vitakatifu. Zaidi ya hilo, unatufanya kuwathamini wengine katika tofauti zao na kuwatambua kuwa kweli kaka zetu na dada zetu.
Kama wanadamu, sisi tuna vitu vingi sana vinavyofanana ambabvyo vinatuwezesha kuishi karibu na kila mmoja wetu, tukizikaribisha tofauti zetu kwa ile furaha ya kuwa kaka na dada. 
Na tuombe ili tofauti ndogo, au tofauti kubwa kama ile ya kidini, isiufanye ule mwungano mkuu wa kuwa kaka na dada usionekane.
Na tuichague njia ya undugu. Kwa sababu ama sisi ni kaka na dada, ama sote tunapoteza.
Tusali ili wale wanaobaguliwa na kukandamizwa kwa sababu za kidini waweze kupata ndani ya jamii wanamoishi haki na heshima ya kiutu inayotokana na kuwa kaka na dada.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – January 2022: Religious discrimination and persecution

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

La Machi Communication for Good Causes

Music production and mix by:

Índigo Music Design

Benefactors

Benefactors:

ACN International

Media partners:

Aleteia

With the Society of Jesus

adminJANUARI | Ubaguzi na ukandamizaji wa kidini