FEBRUARI | Kwa ajili ya Watawa wa Kike na Wanawake Waliowekwa Wakfu

Tuwaombee watawa wa kike na wanawake waliowekwa wakfu, tukiwashukuru kwa utume wao na ujasiri wao; waendelee kupata majibu mapya ya changamoto za nyakati zetu.

Pope Francis – February 2022

Kwa mwezi huu, tutaomba kwa namna ya pekee kwa ajili ya watawa wa kike na wanawake waliowekwa wakfu.
Je, Kanisa lingekuwaje pasipo kuwa na watawa wa kike na wanawake walei waliowekwa wakfu? Kanisa lisingeeleweka bila wao.
Ninawahimiza wanawake wote waliowekwa wakfu watambue na wachague yale yanayofaa zaidi kwa ajili ya utume wao katika kukabiliana na changamoto za malimwengu tunazokumbana nazo.
Ninawasihi waendelee kufanya kazi na kuwa na matokeo chanya kwa maskini, wale wanaotengwa, pamoja na wale wote wanaotumikishwa kwenye utumwa mamboleo; Ninaomba sana muwatetee kwa niaba yao.
Na tuombe ili waonyeshe uzuri wa upendo na huruma ya Mungu kama makatekista, wanatauhidi, na viongozi wa kiroho.
Niwaalike kupambana, pale ambapo, wanawake wanatendewa isivyo haki, hata ndani ya Kanisa; wanamohudumu sana hivi kwamba, hushushwa hadhi na kutumikishwa—wakati mwingine, na wanaume wa Kanisa.
Wasivunjike moyo. Waendelee kuutangaza wema wa Mungu kupitia kazi za kitume wanazozifanya. Lakini zaidi ya yote kupitia ushuhuda wao wa kuwekwa wakfu.
Tuwaombee watawa wa kike na wanawake waliowekwa wakfu, tukiwashukuru kwa utume wao na ujasiri wao; waendelee kupata majibu mapya ya changamoto za nyakati zetu.
Asanteni kwa jinsi mlivyo, kwa kile mnachokifanya, na namna mnavyokifanya.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – February 2022: For religious sisters and consecrated women

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

Gaia Valeria Rosa, Diego Angeli and Andrea Schneider Graziosi

Benefactors

Benefactors:

UISG International Union of Superiors General

Media partners:

Aleteia

Thanks to:

Progetto Chaire Gynai dell’Associazione Scalabriniane con i Migranti
Talitha Kum
Stefano dal Pozzolo
Lisa Kristine
Laudato Si Movement
Fondazione Missio
Pontificia Università Gregoriana
AFP
Congregazione Suore Ministre Degli Infermi di San Camillo

With the Society of Jesus

adminFEBRUARI | Kwa ajili ya Watawa wa Kike na Wanawake Waliowekwa Wakfu