MACHI | Mwitikio wa Kikristo kwenye changamoto za kimaadili-biolojia

Tunawaombea Wakristo wanaokabiliwa na changamoto hizi mpya za kimaadili; waendelee kutetea hadhi ya utu wa maisha yote ya binadamu kwa sala na matendo.

Pope Francis – Machi 2022

Tuombe ili tuweze kutoa jibu la Kikristo kwenye changamoto za maadili-biolojia.
Ni dhahiri kwamba sayansi imeendelea, na leo katika Nyanja za maadili-biolojia unatuletea mfululizo wa matatizo ambayo inatulazimu kuyajibu, si kuficha vichwa vyetu kama mbuni.
Kila wakati ni lazima matumizi ya kibioteknolojia lazima yatumike kwa kuzingatia heshima ya utu wa binadamu.
Kwa mfano, viinitete vya binadamu haviwezi kuzingatiwa kama nyenzo (vitu vya) za kutupwa. Utamaduni huu wa kutupa pia unatumika kwa wingi; haiwezekani, hilo haliwezi kufanywa. Kuendelea kupanua utamaduni kama huo kwa njia hii, unadhuru sana.
Au hata, kuruhusu faida ya kifedha ili kufanya tafiti kama hizo za kimatibabu.
Tunahitaji kuelewa kwa kina mabadiliko makubwa yanayofanyika kwa utambuzi wa kina zaidi na wenye hila.
Hili sio suala la kuzuia maendeleo ya kiteknolojia hata kidogo. Hapana, lazima tuandamane nao. Swala hili linahusu kulinda utu na hadhi ya maendeleo ya binadamu. Hii ni kusema, hatuwezi kugharamia utu wa binadamu kwa ajili ya maendeleo, haiwezekani. Yote mawili yanaenda sawia, lakini kwa muktadha wa maelewano.
Tunawaombea Wakristo wanaokabiliwa na changamoto hizi mpya za kimaadili; waendelee kutetea hadhi ya utu wa maisha yote ya binadamu kwa sala na matendo.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – March 2022: For a Christian response to bioethical challenges

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

La Machi Communication for Good Causes

Music production and mix by:

Índigo Music Design

Benefactors

adminMACHI | Mwitikio wa Kikristo kwenye changamoto za kimaadili-biolojia