APRILI | Kwa Wahudumu wa Afya

Tuwaombee wahudumu wa afya wanaohudumia wagonjwa, na wazee hasa katika nchi maskini zaidi; waungwe mkono vya kutosha na serikali na jumuiya za mitaa.

Pope Francis – April 2022

Mwezi huu tuombe kwa ajili wahudumu wa afya.
Ambo (gonjwa) hili, limetuonyesha majitoleo na ukarimu wa wahudumu wa afya, watu wengi wanaojitolea, wasaidizi maofisini, mapadre, pamoja na watawa wa kike na wa kiume.
Lakini janga hilo pia limefichua ukweli kwamba sio kila mtu anapata mfumo mzuri wa afya ya umma inavyostahili.
Nchi maskini zaidi, na nchi zilizo hatarini zaidi, haziwezi kupata matibabu yanayohitajika kushughulikia magonjwa mengi yanayoendelea kuwasumbua.
Mara nyingi, hii ni kutokana na usimamizi mbaya wa rasilimali na ukosefu wa dhamira kubwa ya kisiasa.
Kwa hiyo, niziombe serikali za nchi zote ulimwenguni, zisisahau kwamba huduma bora za afya, zinazoweza kupatikana kwa wote, ni kipaumbele.
Lakini pia tukumbuke kwamba huduma za afya si shirika tu, bali yategemea majitoleo ya wake kwa waume, wanaojisadaka maisha yao kutunza afya za watu wengine. Na wakati wa janga hili, wengi wametoa maisha yao kusaidia wagonjwa wengi kupona.
Tuwaombee wahudumu wa afya wanaohudumia wagonjwa, na wazee hasa katika nchi maskini zaidi; waungwe mkono vya kutosha na serikali na jumuiya za mitaa.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – April 2022: For Health Care Workers

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

Gaia Valeria Rosa, Diego Angeli and Andrea Schneider Graziosi

Benefactors

Media partners:

Aleteia

Thanks to:

Ordine Ospedaliero di San Giovanni di Dio – Fatebenefratelli (Provincia de España)
Doctors with Africa CUAMM
Fondazione AVSI Uganda
Dr. Erik L. Jennings
Congregazione Suore Ministre degli Infermi di San Camillo
CADIS (Camillian Disaster Service International)
FOCSIV -Volontari nel mondo
COMIVIS Comunità Missionaria di Villaregia
COE Centro Orientamento Educativo
Apurimac ETS

With the Society of Jesus

adminAPRILI | Kwa Wahudumu wa Afya