MEI | Kwa Vijana Waliojaa Imani

Ndugu zangu, tuombe, ili vijana wote walioitwa kuishi maisha yao kikamilifu, kupitia maisha ya Maria, wagundue nyenzo ya usikivu, utambuzi wa kina, ujasiri wa imani, na kujitolea kwa huduma.

Pope Francis – May 2022

Nikizungumzia kuhusu familia, ningependa nianze kwanza kwa kuwaadhi vijana.
Ninapofikiria mfano wa kuigwa, ambaye vijana wangeweza kujilinganisha naye, kinachonijia akilini siku zote ni Mama yetu, Maria: ujasiri wake, usikivu wake, na majitoleo yake katika kutumikia.
Alikuwa hodari na aliazimia kusema “NDIYO” kwa Bwana.
Nyinyi vijana, mnaotaka kujenga kitu kipya, ulimwengu bora, fuateni nyayo zake, kujitosa (kujihatarisha).
Msisahau kwamba ili kufuata nyayo za Maria mnahitaji kutambua na kugundua kile ambacho Yesu anahitaji kutoka kwenu, sio kile mnachofikiria kwamba mnaweza kufanya.
Na katika mang’amuzi haya, mtasaidika sana kusikiliza mawaidha ya [wahenga] babu zetu.
Kwa maneno hayo ya wahenga, mtapata hekima itakayowasaidia zaidi ya masuala ya usasa.
Watawapatia muhtasari wa masuala yanayowahusu.
Ndugu zangu, tuombe, ili vijana wote walioitwa kuishi maisha yao kikamilifu, kupitia maisha ya Maria, wagundue nyenzo ya usikivu, utambuzi wa kina, ujasiri wa imani, na kujitolea kwa huduma.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – May 2022: For Faith-Filled Young People

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

La Machi Communication for Good Causes

Music production and mix by:

Índigo Music Design

adminMEI | Kwa Vijana Waliojaa Imani