JULAI | Kwa ajili ya huduma ya kichungaji kwa wagonjwa

Tusali ili Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa iwape nguvu ya Bwana wale wanaoipokea na wanaowapenda, na pia daima iwe kwa kila mtu alama wazi zaidi ya huruma na matumaini.

Baba Mtakatifu – JULAI 2024

Mwezi huu, tusali kwa ajili ya huduma ya kichunguji kwa wagonjwa
Mpako wa Wagojwa si sakramenti kwa ajili ya wale tu walio karibu ya kufa. Hapana—Ni muhimu jambo hili likiwekwa sawa.
Kuhani anapomkaribia mtu ili afanye Mpako wa Wagonjwa, si lazima awe akimsaidia kuyaacha maisha haya. Kufikiria namna hiyo kuna maana ya kupoteza tumaini kabisa.
Maana yake ni kudhani kuwa baada ya kuhani kuondoka, watakaowasili ni wafanyao maziko.
Tukumbuke kuwa Mpako wa Wagonjwa ni moja ya “sakramenti za uponyaji,” sakramenti zinazohuisha au kuponya roho.
Pale mtu anapokuwa mgojwa sana, inashauriwa apawe Mpako wa Wagonjwa. Pia mtu anapokuwa mzee sana, ni vema apate Mpako wa Wagonjwa.
Tusali ili Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa iwape nguvu ya Bwana wale wanaoipokea na wanaowapenda, na pia daima iwe kwa kila mtu alama wazi zaidi ya huruma na matumaini.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – JULY | For the pastoral care of the sick

A project by  the Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with  Vatican Media

Creativity and co-production by:

Anointing of the Sick, Sacrament, Hope, The Pope Video, Prayer Intention, Click To Pray, We Pray Together, Holy Spirit, Vatican, Church, Catholic

fiorellaJULAI | Kwa ajili ya huduma ya kichungaji kwa wagonjwa