Tusali ili kwamba wahamiaji wanaokimbia vita au njaa, wanaolazimika kufunga safari wakipambana na hatari na vurugu nyingi, wapate nafasi mpya ya kuishi.
Baba Mtakatifu – JUNI 2024
Ndugu wapendwa, mwezi huu napenda tuwaombee watu wanaozikimbia nchi zao.
Hisia za kung’olewa au kutokujua wapi hasa ni nyumbani huendana na machungu wanayopitia watu wanaolazimika kukimbia makwao kwa sababu ya vita na umasikini.
Zaidi ya hayo, katika baadhi ya nchi wanazoelekea, wakimbizi huonekana kama vile tishio na kuogopwa.
Kisha kuta zinazuka, kuta zinazotenganisha familia, na kuta ndani ya mioyo ya watu.
Wakristo hawawezi kukubaliana na mwonekano huo. Yeyote anayemkaribisha mhamiaji anamkaribisha Kristo.
Sharti tujenge utamaduni wa kijamii na kisiasa ambao unalinda haki na heshima ya wahamiaji, utamaduni unaowaongezea uwezekano wa kufikia upeo wa juu kabisa wa matumizi ya karama zao.
Mhamiaji anahitaji kusaidiwa, kupewa fursa ya maendeleo na kukubaliwa katika jamii.
Tusali ili kwamba wahamiaji wanaokimbia vita au njaa, wanaolazimika kufunga safari wakipambana na hatari na vurugu nyingi, wapate nafasi mpya ya kuishi.
Credits
Campaign title:
The Pope Video – JUNE | For those fleeing their own countries
A project by Pope’s Worldwide Prayer Network
In collaboration with Vatican Media
Creativity and co-production by:
Benefactors
Migrants, War, Poverty, Refugees, The Pope Video, Prayer Intention, Click To Pray, We Pray Together, Holy Spirit