Kaka na dada, tuombe kila mtu aliyebatizwa ajihusishe na uinjilishaji, na awe tayari kwa utume, kwa kuwa mashahidi wa maisha ambayo yana ladha ya Injili.
Pope Francis – October 2021
Yesu anatuomba sisi sote, na wewe pia, kuwa wanafunzi wamisionari. Je, upo tayari?
Inatosha kuwa tayari ili kuitikia wito wake na kuishi ukiwa umeungana na Bwana kwa vitu vya kawaida kabisa vya kila siku—kazi, kukutana na watu wengine, kazi zetu za kila siku, nafasi za matukio ya kila siku–tukikubali daima kuongozwa na Roho Mtakatifu.
Kama Kristo anakugusa, kama unafanya mambo kwa sababu Kristo anakuongoza, wengine wataona kwa urahisi.
Na ushuhuda wako wa maisha utavutia, na mvuto utawapa wengine msukumo wa kujiuliza “Inawezekanaje kwa mtu huyu kuwa namna hii”: au nini chanzo cha upendo ambacho mtu huyu anamtendea kila mmoja—upole na ucheshi mzuri?”
Tukumbuke kuwa utume si kushawishi watu wabadili dini; utume una msingi wake katika kukutana kati ya watu, kwenye ushuhuda wa wanaume na wanawake ambao wanasema, “ninamjua Yesu, na ningelipenda na wewe pia umjue.”
Ndugu zangu tuombe ili kila aliyebatizwa aweze kujihusisha na uinjilishaji, awe tayari kwa utume kwa kuwa shahidi wa maisha ambayo yana ladha ya Injili.
Credits
Campaign title:
The Pope Video – October 2021: Missionary Disciples
A project by Pope’s Worldwide Prayer Network
In collaboration with Vatican Media
Creativity and co-production by:
La Machi Communication for Good Causes
Music production and mix by:
Benefactors
Wanafunzi wamisionari, ushuhuda wa maisha, Injili, misheni, kumjua Yesu, uinjilishaji.