Tuombe ili sote tufanye maamuzi yenye ujasiri, maamuzi yaliyo ya lazima kwa maisha endelevu ya mazingira, tukichukua msukumo kutoka kwa vijana wetu ambao kwa uthabiti wamejotolea kwa ajili ya mazingira.
Pope Francis – Septemba 2021
Ninafurahi sana kuwaona vijana wakiwa na ujasiri wa kuanzisha miradi kwa ajili ya mazingira na kuboresha jamii, kwa kuwa hivi viwili vinakwenda pamoja.
Sisi watu wazima tunaweza kujifunza mengi kutoka kwao, kwa sababu katika mambo yote yanayohusiana na sayari (dunia), wao wapo mstari wa mbele.
Tuutumie vizuri mfano wao na kuutafakari mtindo wao wa maisha, hasa nyakati hizi za migogoro ya afya, jamii na ya kimazingira.
Tutafakari namna tunavyokula, tunavyojinunulia, tunavyosafiri, au tunavyotumia maji, nishati, plastiki, na vitu vingine vingi, mara nyingi ni hatari kwa dunia.
Tuchague kubadilika! Tusonge mbele na vijana kuelekea kwenye mitindo ya maisha ambayo ni rahisi zaidi na inayoheshimu zaidi mazingira.
Tuombe ili sote tufanye maamuzi yenye ujasiri, maamuzi yaliyo ya lazima kwa maisha endelevu ya mazingira, tukichukua msukumo kutoka kwa vijana wetu ambao kwa uthabiti wamejotolea kwa ajili ya mazingira. Na si wajinga kwa sababu wamejitolea kwa sababu ya siku zao za baadaye. Ndio maana wanataka kubadili kile watakachokirithi wakati ambao hatutakuwepo.
Credits
Campaign title:
The Pope Video – September 2021: An Environmentally Sustainable Lifestyle
A project by Pope’s Worldwide Prayer Network
In collaboration with Vatican Media
Production house:
Produced by:
Sam Barton-Humphreys
Directed by:
Nicolas Brown
Creativity and co-production by:
La Machi Communication for Good Causes
Music production and mix by:
Benefactors
Benefactors:
Media partners:
Thanks to:
Dicastery for Promoting Integral Human Development
Laudato Si’ Movement
Doppler Email Marketing
With the Society of Jesus
Mazingira, mtindo wa maisha endelevu wa kimazingira, uendelevu, mtindo wa maisha endelevu, miradi ya kimazingira, ekolojia.