NOVEMBA | Watu wanaosumbuliwa na mfadhaiko

Tuombe ili watu wanaosumbuka na majonzi au waliochoka watapate msaada na mwanga ambao utawaangazia maisha.

Pope Francis – November 2021

Kufanya kazi kupita kiasi na msongo unaoambatana na kazi vinasababisha watu wengi kuwa na uchovu uliopindukia— akili, jazba, hisia, na uchovu wa mwili.
Na bila shaka, kwa saababu hiyo, majonzi, kutokujali, na uchovu wa kiroho vinaishia kuyatawala maisha ya watu, ambayo yameelemewa kutokana na mtindo wa sasa wa maisha.
Tujaribu kujitahidi kuwa karibu na wale waliochoka, waliokata tamaa na wasiyo na matumaini. Mara nyingi tusikilize katika ukimya kwa sababu hatuwezi kwenda kumwambia mtu, ‘Hapana, maisha hayapo hivyo. Nisikilize mimi, nitakupa maelekezo.’ Hakuna maelekezo.
Mbali na hilo, tusisahau kwamba pamoja na mwongozo muhimu wa mwanasaikolojia, ambao ni wa manufaa na ufanisi, maneno ya Yesu pia yanasaidia. Maneno haya yamenijia kwenye fikra zangu na moyo wangu: ‘Njoni nyote mnaoelemewa na mizigo mizito nami nitawapumzisha.’
Tuombe ili watu wanaosumbuka na majonzi au waliochoka watapate msaada na mwanga ambao utawaangazia maisha.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – November 2021: People who suffer from depression

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

La Machi Communication for Good Causes

Music production and mix by:

Índigo Music Design

Benefactors

Benefactors:

Association of Catholic Mental Health Ministers

Media partners:

Aleteia

Thanks to:

Francisco Segarra Alegre

With the Society of Jesus

Mfadhaiko, wasiwasi, uchovu uliopitiliza, uchovu, uchovu wa kiroho, tiba ya kisaikolojia, ugonjwa wa akili.

adminNOVEMBA | Watu wanaosumbuliwa na mfadhaiko