Tuwaombee watoto wanaoteseka hasa wale wasio na makazi, yatima, na wahanga wa vita. Wapate uhakika wa kupata elimu na wawe na fursa ya kupata upendo wa familia.
Pope Francis – November 2022
Bado kuna mamilioni ya wavulana na wasichana wanaoteseka na kuishi katika hali zinazofanana sana utumwa.
Wao sio “manamba”: Ni wanadamu wenye majina, wenye sura yao wenyewe, na utambulisho ambao Mungu amewapa.
Mara nyingi, tunasahau wajibu wetu na tunafunga macho yetu kwa ugandamizwaji wa watoto hawa ambao hawana haki ya kucheza, kusoma, kuota ndoto za maisha yao. Hawafurahii hata kidogo joto la familia.
Kila mtoto aliyetengwa, aliyeachwa na familia yake, bila shule, bila afya, ni kilio! Kilio kinachoinuka mpaka kwa Mungu na kuuaibisha mfumo ambao sisi watu wazima tumeujenga.
Mtoto aliyeachwa ni kosa letu.
Hatuwezi tena kuwaruhusu wahisi upweke na walioachika—wana haki ya kupata elimu na kuhisi upendo wa familia ili wajue kwamba Mungu hajawasahau.
Tuwaombee watoto wanaoteseka hasa wale wasio na makazi, yatima, na wahanga wa vita. Wapate uhakika wa kupata elimu na wawe na fursa ya kupata upendo wa familia.
Credits
Campaign title:
The Pope Video – November 2022: For children who suffer
A project by Pope’s Worldwide Prayer Network
In collaboration with Vatican Media
Creativity and co-production by:
Gaia Valeria Rosa, Diego Angeli and Andrea Schneider Graziosi