APRILI | Kwa utamaduni wa amani na usio na vurugu

Na tuombe kwa ajili ya kuenea zaidi kwa utamaduni wa kutotumia mabavu, ambao unahusisha utumiaji mdogo wa silaha, kwa serikali na raia.

Pope Francis – April 2023

Kuishi, kuzungumza na kutenda bila jeuri haimaanishi kukata tamaa, kupoteza au kuacha chochote. Inamaanisha kutamani kila kitu.
Kama Mtakatifu John XXIII alivyosema miaka 60 iliyopita katika waraka kumbakumba Pacem in Terris, (Amani Ulimwenguni) vita haina mantiki, ni zaidi ya kutofikiri.
Vita yoyote, mapigano yoyote ya silaha, daima huisha kwa wote kushindwa.
Tujenge utamaduni wa amani.
Tukumbuke hata katika kujilinda, amani ndio lengo kuu. Na kwamba amani ya kudumu inaweza tu kuwa amani isiyo na silaha.
Hebu tusifanye vurugu katika maisha ya kila siku na katika mahusiano ya kimataifa, huu uwe mwongozo wa matendo yetu.
Na tuombe kwa ajili ya kuenea zaidi kwa utamaduni wa kutotumia mabavu, ambao unahusisha utumiaji mdogo wa silaha, kwa serikali na raia.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – April 2023: For a non-violent culture

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

La Machi Communication for Good Causes

Music production and mix by:

Índigo Music Design

Benefactors

Peace, Non-violence, Disarmament, Culture of Non-violence, What is Non-violence, Armed confrontations, Self-defens.

adminAPRILI | Kwa utamaduni wa amani na usio na vurugu