MACHI | Kwa waathiriwa wa unyanyasaji

Tuwaombee wale ambao wameteseka kwa sababu ya maovu waliyotendewa kutoka kwa washirika wa Kanisa; wapate ndani yao Kanisa lenye jibu thabiti kwa mateso na maumivu yao.

Baba Mtakatifu – Machi 2023

Katika kukabiliana na kesi za unyanyasaji, hasa kwa wale waliotendewa na washiriki wa Kanisa, haitoshi kuomba msamaha.
Kuomba msamaha ni muhimu, lakini haitoshi. Kuomba msamaha ni vyema kwa ajili ya waathirika, lakini wao ndio wanapaswa kuwa “katikati” ya kila kitu.
Maumivu yao na majeraha yao ya kisaikolojia yanaweza kuanza kupona ikiwa watapata majibu—ikiwa zipo hatua madhubuti za kurekebisha maovu waliyoyapata na kuyazuia yasitokee tena.
Kanisa haliwezi kujaribu kuficha janga la unyanyasaji wa aina yoyote. Hata kama unyanyasaji unafanyika katika familia, kwenye vilabu, au kwenye aina nyiginezo za taasisi.
Kanisa lazima liwe kielelezo cha kusaidia kutatua suala hilo na kuliweka wazi katika jamii na ndani ya familia.
Kanisa lazima litoe nafasi salama kwa waathirika kusikilizwa, kusaidiwa kisaikolojia, na kulindwa.
Tuwaombee wale ambao wameteseka kwa sababu ya maovu waliyotendewa kutoka kwa washirika wa Kanisa; wapate ndani yao Kanisa lenye jibu thabiti kwa mateso na maumivu yao.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – March 2023: For victims of abuse

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

Gaia Valeria Rosa, Diego Angeli and Hermes Mangialardo.

Illustrations by:

Hermes Mangialardo

Victims, Abuse, Victims of abuse, Helping victims, Abuse of an kind, Refuge, Church.

adminMACHI | Kwa waathiriwa wa unyanyasaji