JUNI | Ili huruma iongezeke ulimwenguni

Tusali ili kwamba kila mmoja wetu apate faraja katika uhusiano binafsi na Yesu, na kutoka katika Moyo wake Mtakatifu, ajifunze kuuhurumia ulimwengu.

(Papa Leo XIV)

Bwana, leo hii naujia Moyo Wako mpole,
nakujia Wewe mwenye maneno yawashayo moto moyoni mwangu,
nakujia Wewe unayemimina huruma kwa walio wadogo na maskini,
kwa wenye kuteseka, na juu ya taabu zote za wanadamu.

Natamani kukujua Wewe zaidi, kukutafakari Wewe katika Injili,
kuwa Nawe na kujifunza kutoka Kwako
na kutoka katika upendo wako unaokufanya Wewe ukubali
kuguswa na kila aina ya umaskini.

Ulituonesha upendo wa Baba kwa kutupenda bila kipimo
kwa Moyo Wako wa Kimungu na kibinadamu

Wajalie watoto Wako wote neema ya kukutana Nawe.
Badilisha, tengeneza na fanya upya mipango yetu,
Ili kwamba tukutafute Wewe pekee katika kila hali:
katika sala, katika kazi, katika mazungumzo na katika ratiba zetu za kila siku.

Kutokana na mazungumzo haya, tupeleke kwenye utume,
utume wa huruma kwa ulimwengu
ambamo Wewe ndiwe chemchemi ya faraja zote.

Amina.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – JUNE | That the world might grow in compassion

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

adminJUNI | Ili huruma iongezeke ulimwenguni