JANUARI: Kwa huduma ya udugu wa Binadamu

Tuombe ili Bwana atupe neema ya kuishi katika ushirika kamili na kaka na dada zetu wa dini nyingine na si kugombana, bali kuombeana, na kuwa wazi kwa wote.

Pope Francis – January 2021

Tunapomuomba Mungu kumfuata Yesu, tunaungana pamoja kama kaka na dada na wale ambao wanasali kulingana na tamaduni nyingine, mila nyingine na imani nyingine.
Sisi ni kaka na dada ambao tunasali.
Udugu unatuongoza kujifungua kwa Baba wa wote na kuona kwa mwingine kaka au dada, kushirikishana maisha yetu au kusaidiana, kupendana na kujuana.
Kanisa linathamini matendo ya Mungu kwa wengine na kwa dini nyingine, bila kusahau kwamba kwetu sisi Wakristo, chanzo cha utu wa mwanadamu na udugu kipo katika Injili ya Yesu.
Sisi waamini ni lazima turudi kwenye vyanzo vyetu na kuleta pamoja kilicho muhimu. Kilicho muhimu kwa imani yetu ni kumwabudu Mungu na kumpenda jirani.
Tuombe ili Bwana atupe neema ya kuishi katika ushirika kamili na kaka na dada zetu wa dini nyingine na si kugombana, bali kuombeana, na kuwa wazi kwa wote.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – January 2021: At the service of Human fraternity

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

La Machi Communication for Good Causes

Music production and mix by:

Índigo Music Design

Benefactors

adminJANUARI: Kwa huduma ya udugu wa Binadamu