Novemba: KWA AJILI YA AMANI

Tusali pamoja ili lugha ya upendo na majadiliano iweze daima kuishinda lugha ya vurugu.

Pope Francis – November 2018

Sote tunahitaji amani. Amani inahitajika zaidi kwa wale ambao wanahangaikia kutokuwepo kwake.
Tukumbuke kwamba Bwana Wetu Yesu pia aliishi nyakati za vurugu. Yesu alitufundisha kuwa amani ya kweli imo ndani ya moyo wa mwanadamu.
Tunaweza kuongea maneno mazuri, lakini kama hakuna amani ndani ya mioyo yetu, hakutakuwa na amani duniani.
Tuifanyie kazi amani katika vitu vidogovidogo, na turuhusu majadiliano yaongoze mahusiano yetu binafsi na mahusiano ya kijamii.
Kwa kutokuwepo na vurugu na asilimia mia moja ya wema, tujenge amani ya kiinjili ambayo haimtengi yeyote, bali humjumuisha kila mmoja hasa vijana na Watoto.
Tusali pamoja ili lugha ya upendo na majadiliano iweze daima kuishinda lugha ya vurugu.

adminNovemba: KWA AJILI YA AMANI