AGOSTI | Kwa ajili ya viongozi wa kisiasa

Tuwaombee viongozi wa kisiasa wawe kwa ajili ya kuwatumikia watu wao, wafanye kazi kwa ajili ya maendeleo kamili ya mwanadamu na kwa manufaa ya wote, wakiwajali wale waliopoteza ajira zao na kutoa kipaumbele kwa walio maskini zaidi.

Baba Mtakatifu – Agosti 2024

Leo, siasa haina sifa nzuri: ufisadi, kashfa, kutojihusisha na maisha ya kila siku ya watu.
Lakini je, tunaweza kuendelea mbele katika kujenga udugu wa wote ulimwenguni bila siasa nzuri? Hapana.
Kama Papa Paulo wa Sita alivyosema, siasa ni moja kati ya aina za juu sana za hisani kwa kuwa inatafuta manufaa ya wote.
Hapa nazungumzia SIASA nikitumia herufi kubwa, wala si kupiga-siasa. Nazungumzia siasa inayosikiliza kile hasa kinachotukia, iliyo kwa ajili ya huduma kwa maskini, na siyo aina ya siasa inaiyojificha kwenye majumba makubwa na kumbi za kifahari.
Nazungumzia siasa inayowajali wasio na ajira, na inayojua vizuri kabisa jinsi ilivyo Jumapili ikiwa Jumatatu ni siku mojawapo ya kutokuwa na ajira.
Tukiiangalia namna hiyo, siasa huwa nzuri zaidi kuliko inavyoonekana.
Tuwe na shukrani kwa wanasiasa wengi wanaotekeleza majukumu yao kwa nia ya kutumikia, si ya kutafuta madaraka, wanaoweka juhudi zao zote kwa manufaa ya wote.
Tuwaombee viongozi wa kisiasa wawe kwa ajili ya kuwatumikia watu wao, wafanye kazi kwa ajili ya maendeleo kamili ya mwanadamu na kwa manufaa ya wote, wakiwajali wale waliopoteza ajira zao na kutoa kipaumbele kwa walio maskini zaidi.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – AUGUST | For political leaders

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

Benefactors

Politics, Service, Leaders, Leadership, Unemployment, Charity, Common Good, The Pope Video, Prayer Intention, Click To Pray

adminAGOSTI | Kwa ajili ya viongozi wa kisiasa