Tusali ili kila mmoja wetu asikilize kwa moyo kilio cha Dunia yetu, na cha wahanga wa majanga ya kimazingira na mabadiliko ya hali ya hewa, tukijitoa binafsi kutunza ulimwengu tunamoishi.
Baba Mtakatifu – Septemba 2024
Tusali kwa ajili ya kilio cha Dunia.
Kama tukiangalia joto la sayari yetu, tutaambiwa kuwa Dunia ina homa. Na kuwa inaumwa, kama ilivyo kwa yeyote aliye mgonjwa.
Lakini je, tunayasikiliza maumivu haya?
Tunasikia maumivu ya mamilioni ya wahanga wa majanga ya kimazingira?
Wanaoteseka zaidi kutokana na matokeo ya majanga haya ni maskini, wale wanaolazimika kuacha makazi yao kwa sababu ya mafuriko, mawimbi ya joto na ukame.
Kukabiliana na migogoro ya kimazingira inayosababishwa na binadamu, kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, uchafuzi wa mazingira na upotevu wa viumbe hai, kunahitaji mwitikio ambao si wa kiikolojia pekee, bali pia wa kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Sharti tujitoe kabisa kupambana dhidi ya umaskini, na tujibidiishe kulinda maliasili, huku tukibadili tabia zetu binafsi na za jamii.
Tusali ili kila mmoja wetu asikilize kwa moyo kilio cha Dunia yetu, na cha wahanga wa majanga ya kimazingira na mabadiliko ya hali ya hewa, tukijitoa binafsi kutunza ulimwengu tunamoishi.
Credits
Campaign title:
The Pope Video – SEPTEMBER | For the cry of the Earth
A project by Pope’s Worldwide Prayer Network
In collaboration with Vatican Media
Creativity and co-production by:
Gaia Valeria Rosa y Diego Angeli
Benefactors
Global Crisis, Earth, Ecology, Environment, Fight, Commitment, The Pope Video, Prayer Intention, Click To Pray