AGOSTO | Kanisa Njiani

Tuliombee Kanisa ili liweze kupokea neema na nguvu za Roho Mtakatifu liweze kujirekebisha kulingana na Injili.

Pope Francis – Agosto 2021

Utume halisi wa Kanisa ni uinjilishaji, ambao si ushawishi wa kubadili dini, hapana. Utume wake ni uinjilishaji. Zaidi ya hapo, utambulisho wa Kanisa ni Uinjilishaji.
Tunaweza tu kulipa moyo Kanisa kwa kutambua mapenzi ya Mungu katika maisha yetu ya kila siku na kuanzisha mabadiliko yanayoongozwa na Roho Mtakatifu. Uongofu wetu sisi kama watu ni yale mabadiliko. Ni lazima tumruhusu Roho Mtakatifu, aliye zawadi ya Mungu katika mioyo yetu, kutukumbusha aliyotufundisha Yesu na kutusaidia kuyaweka katika matendo.
Tuanze kulifanyia mageuzi Kanisa kwa kuanza na mageuzi yetu sisi wenyewe, bila ya mawazo yaliyotungwa, bila ya upendeleo wa kiitikadi, bila kuweka ugumu, bali kusonga mbele kulingana na tajriba ya kiroho, tajriba ya sala, tajriba ya huruma, tajriba ya huduma.
Ninaota zaidi juu ya aina nyingine ya chaguo la kimisionari; ambalo linakwenda kukutana na wengine bila ya kuwashawishi kubadili dini na kwamba linalofanyia mabadiliko miundo yake yote kwa ajili ya uinjilishaji wa dunia ya sasa.
Tukumbuke kwamba Kanisa siku zote lina dhiki, lina migogoro, kwa sababu lipo hai. Vitu vilivyo hai hupatwa na migogoro. Vitu vilivyo kufa ndivyo pekee havina migogoro.
Tuliombee Kanisa ili liweze kupokea neema na nguvu za Roho Mtakatifu liweze kujirekebisha kulingana na Injili.

Credits

Campaign title:

The Pope Video – August 2021: Church on the Way

A project by Pope’s Worldwide Prayer Network

In collaboration with Vatican Media

Creativity and co-production by:

Gaia Valeria Rosa, Diego Angeli and Andrea Schneider Graziosi

Music production and mix by:

Índigo Music Design

adminAGOSTO | Kanisa Njiani